Wednesday, December 31, 2008

Mwambusi ateuliwa kuinoa Simba

KOCHA wa zamani wa Prisons ya Mbeya, Juma Mwambusi, ameteuliwa kuinoa timu ya Simba ya Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya klabu hiyo mjini Dar es Salaam jana, zilisema kocha huyo atainoa timu hiyo kwa mashindano ya Kombe la Mapinduzi linalotarajia kuanza mwishoni mwa wiki mjini Zanzibar.

Kocha huyo atasaidiana na Amri Said wakati jitihada za kumpata kocha mpya wa kigeni zikiendelea.

"Tumemchukua Mwambusi na kesho (leo), tutamtambulisha rasmi na ataanza mara moja kazi ya kukinoa kikosi," kilisema chanzo cha habari hii.

Chanzo hicho kilidai kuwa Simba imeachana na suala la mserbia Milovan Cirkovic na kufanya mazungumzo na Patrick Phiri wa Zambia, na makocha wengine wa Ureno na Ujerumani.

Kilisema katika mazungumzo ya awali, Phiri ameonyesha nia ya kurejea Msimbazi.

No comments:

Post a Comment