Sunday, December 7, 2008

Liverpool yajikita kileleni

Magoli yaliyofungwa na Xabi Alonso, Yossi Benayoun na Steven Gerrard yalitosha kuiweka Liverpool kileleni mwa ligi ya Uingereza na kuiacha Blackburn Rovers njia panda baada ya kucheza mechi 10 bila ya ushindi.

Kocha Paul Ince alionekana kuchanganyikiwa baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo huo huku washabiki wenye hasira wakimzomea kutokana na maendeleo dhaifu ya Blackburn Rovers.

Blackburn walikianza kipindi cha kwanza kwa kasi , wakicheza kwa kuelewana zaidi na kumiliki eneo la kiungo na kuifanya Liverpool kucheza zaidi winga za pembeni. Hadi mapumziko hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake.

Kipindi cha pili Liverpool waliweza kuibana zaidi Blackburn katika idara ya kiungo baada ya kuvunja winga moja na kuweka viungo zaidi.

Liverpool walifanikiwa kupata goli katika dakika ya 69 bao safi kutoka kwa Xabi Alonso. Iliwachukua dakika kumi Liverpool kuandika bao la pili lililofungwa na Yossi Benayoun.

Baada ya bao hilo Blackburn ilitulia na kuanza kucheza mipira mirefu zaidi na kunako dakika ya 86 iliweza kupata bao zuri la kichwa lililofungwa na Santa Cruz.

Steve Gerrard aliihakikishia ushindi Liverpool alipoandika goli la tatu katika dakika ya 90.

Matekeo mengine ya mechi zilizochezwa jana ni kama ifuatavyo:
Arsenal 1- 0 Wigan Athletics
Bolton W. 0- 2 Chelsea
Newcastle U. 2- 2 Stoke City
Hull City 2- 1 Middlesborough
Fulham 1-1 Manchester City

Manchester United 1-0 Sunderland

No comments:

Post a Comment