Friday, December 26, 2008

Mawaziri 'wajisalimisha' Guinea



Wanajeshi nchini Guinea waliofanya mapinduzi mapema wiki hii wanaonekana kuimarisha udhibiti katika madaraka.

Mawaziri, ambao ni raia ikiwa ni pamoja na waziri mkuu Ahmed Tidiane Souare wamefika katika kituo cha kijeshi mjini Conakry, kufuatia amri iliyotolewa na kiongozi wa mapinduzi Kapteni Moussa Dadis Camara.

Mawaziri hao waliondoka katika kituo hicho baada ya kuzungumza na wanajeshi.

Mwandishi wa BBC wa Afrika Magharibi anasema mapinduzi hayo, yaliyotokea baada ya kifo cha rais Lansana Conte siku ya Jumatatu, yamepokelewa vizuri na baadhi ya watu nchini Guinea waliokuwa wamechoshwa na utawala wa kimamlaka.

Umoja wa Afrika umelaani mapinduzi hayo, huku umoja wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi ukitarajiwa kupeleka wajumbe wake huko siku ya Jumatatu.


Source: BBC

No comments:

Post a Comment