Nemaja Vidic amefanikiwa kuibuka shujaa wa mchezo baada ya kuifungia Man United goli muhimu katika dakika ya 90 ya mechi ya leo dhidi ya Sunderland ambayo kocha wake Roy Keane alijiuzulu siku tatu zilizopita.
Sunderland muda wote ilikuwa ikicheza wachezaji wote kumi nyuma katika moja ya mbinu ya kulinda lango lao.
Timu zote mbili ziliingia uwanjani bila makocha wao baada ya Roy Keane wa Sunderland kujiuzulu na kocha wa Man United Sir Alex Furguson kugeuka mtazamaji wa kawaida juu ya jukwaa kuu akitimiza adhabu zake alizopewa na chama cha FA.
Katika kipindi cha kwanza man united walipoteza nafasi nyingi za wazi kutoka kwa Berbatov,Fletcher, Ronaldo na Park hali iliyopelekea kwenda mapumziko bila ya kufungana.
Katika kipindi cha pili Man United waliweza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la Sunderland lakini beki ya timu hiyo ilicheza kwa makini ikiongozwa na Anton Ferdinand na kipa Marton Fulop ambaye jana alionekana kuwa nyota wa mchezo baada ya kuokoa michomo mingi ya washambuliaji wa Man United.
Timu zote mbili zilifanya mabadiliko Man United ikiwaingiza Giggs na Anderson kuchukua nafasi za Ronaldo na Fletcher, Sunderland ilifanya mabadiliko kwa kumuingiza Jones kuchukua nafasi ya Cisse.
Mabadiliko hayo yalizaa matunda kwa upande wa United kupata goli la ushindi katika dakika za majeruhi za mchezo huo.
Matokeo hayo yanaifanya Sunderland kushika nafasi ya pili kutoka mkiani ikijikusanyia pointi zake 15 baada ya michezo 16 iliyokwishacheza mpaka sasa.
Introducing Celebration E-Cards: Your Digital Connection Hub
-
We are excited to introduce to you, Celebration E-Cards—an ecards online
platform designed to bridge the gap between heartfelt celebrations and the
ease of...
5 weeks ago
No comments:
Post a Comment