Saturday, December 6, 2008

Mchungaji azua mtafaruku baada ya kuamua kubadilisha jinsia

Mchungaji aliyeamua kufanya upasuaji ili awe mwanamke amezua mtafaruku na kuacha watu wakijiuliza aendelee na uchungaji baada ya upasuaji au la.

Olli Aalto mwenye miaka 55, mchungaji kwa miaka 30 katika kanisa moja la Lutheran katika mji wa Imatra kusini mashariki mwa Finland amezua mtafaruku baada ya kutangaza mpango wake wa kubadili jinsia kuwa mwanamke.

Askofu mkuu Veikko Huottari ambaye mwanzo alisema Aalto hawezi kurudia kazi yake ya uchungaji iwapo atabadilisha jinsia, aliwagawanya waumini kiasi cha kuamua kurudisha uamuzi wake nyuma.

Wakati baadhi ya wananchi wakiunga mkono kuendelea kwa bwana Aalto kuliongoza kanisa kama mwanamke,wananchi wengine wamepinga kabisa hatua hiyo.Aalto ana watoto wawili na amewahi kuoa mara mbili.

Viongozi kadhaa wa kanisa la mchungaji Aalto wameamua kujiuzulu hali iliyopelekea makundi ya kutetea usawa kwa jinsia zote kuingilia kati na kusema "Hakuna sheria inayoruhusu mtu kufukuzwa kazi kwasababu ya kubadilisha jinsia yake".

Mtafaruku huo ulipelekea Askofu mkuu kurudisha uamuzi wake nyuma kutokana na upinzani mkubwa alioupata kutoka kwa watetezi wa haki sawa kwa jinsia zote na kuamua kumuachia mchungaji Aalto kuendelea kuliongoza kanisa.

Mke wa zamani wa mchungaji Aalto anaunga mkono uamuzi wake wa kubadilisha jinsia kuwa mwanamke.

3 comments:

  1. Huyu Hafai hata Kuliongoza kanisa tena! Sasa sijuwi birth certificate yake kama itabadilishwa jinsia??!@#$%^&*

    ReplyDelete
  2. Fala tu! anatudhalilisha midume!-Eric

    ReplyDelete
  3. Tai Ukiweka habari siku nyingine weka link uonyeshe ulikoitoa hiyo habari itaonyesha kuwa unathamini muda wao wape credit zao nifahamishe.com

    ReplyDelete