Monday, December 1, 2008

Italy kuongeza kodi ya ngono ili kuongeza pato la taifa

Msukosuko wa fedha duniani unazisumbua nchi nyingi kiasi cha kufikiria kuongeza kodi katika maeneo yote wanayohisi hayana umuhimu.

Rais Silvio Berlusconi ameamua kuweka kodi maalumu katika mitandao ya picha na sanaa zozote zinazohusiana na picha za ngono. Muswada huo ambao umepitishwa na baraza la mawaziri la Italy ili kukabiliana na msukosuko wa fedha unaoukabili Italy, umepandisha kodi hadi asilimia 25 kwa magazeti na majarida ya picha za ngono,dvd na vyote vyenye kuhusisha picha za ngono. "Kodi ya ngono" ilipendekezwa kwa mara ya kwanza mwaka 2002 na Vittorio Emanuele Falsita aliyekuwa mwakilishi wa chama cha siasa cha Forza Italia (Nguvu ya Italia)kilichoanzishwa na Berlusconi mwaka 1994 lakini mapendekezo hayo hayakupitishwa. Hata hivyo sheria hiyo itajadiliwa tena na tume maalumu ndani ya miezi miwili ili kuweka wazi vitakavyojumuishwa katika kundi la "kodi ya ngono".

No comments:

Post a Comment