Rais Jakaya Kikwete amekerwa na kuudhiwa na taarifa kuwa watuhumiwa wa kesi za kutia mimba wanafunzi, hawawezi kuwajibishwa kutokana na ushahidi wake kuwa mgumu kupatikana.
Kutokana na taarifa hiyo kiongozi huyo wa nchi amewataka viongozi waache kufanya mambo kizamani na badala yake washughulikie tatizo hilo kisasa zaidi.
Amesema tatizo ni kwamba shughuli nyingi za maendeleo zinaendeshwa kizamani hali ambayo katika mazingira ya sasa haiwezekani.
"Kwa kuwa hali hii inaniudhi na sitaki iendelee kuzungumzwa nataka vitendo viwepo kukomesha hali hii," alisema.
Alisema maelezo anayopewa kila mara kwamba mazingira ni tatanishi yanamuonyesha wazi kuwa viongozi wanafanya kazi katika staili ya kizamani wakati nchi imejenga uwezo wa kutosha wa kuwezesha kubanwa kwa mhalifu kwa kupitia utaalamu wa vinasaba (DNA).
Aliwataka waendesha mashitaka kutumia njia hizo za kisasa kukabiliana na tatizo la kutia mimba wasichana badala ya kuacha kwa sababu eti hakuna ushahidi. Rais alisema hakuna ushahidi mwingine kama wa mtoto, ambaye sampuli yake ya DNA lazima irandane na baba anayehusika.
Alisema ushahidi huo unaweza kupatikana kwa uthabiti wake kutokana na kuwapo kwa teknolojia hiyo nchini. Aliyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati akipokea taarifa za maendeleo kwa Wilaya ya Morogoro, Manispaa ya Morogoro na Mvomero.
Alisema kama itabainika kwamba mpango ulisukwa wa kumtaja mtu ambaye hakuhusika na sampuli zikadhihirisha si yeye, basi binti ni lazima abanwe amtaje mhusika hata kama alishafanya mapenzi na watu kadhaa bila ya yeye kujua kwamba nani amempachika mimba.
Alisema ikibainika kwamba binti anasema uongo, sheria lazima ichukue mkondo wake kwa binti kuidanganya mahakama.
Aliyasema hayo kwa mkazo, akisema anashangazwa na idadi ya wanafunzi wanaopata mimba, tena wengi wakiwa shule za msingi na kusema sasa tabia hiyo lazima ikomeshwe kwa kutumia upimaji vinasaba kwani ndio njia pekee ya kweli na wazi ambayo haina ubishi katika ushahidi.
Meta Unveils Edits: A Video Editing App for Creators
-
Meta, the parent company of Facebook and Instagram, is making waves once
again with the announcement of its new video editing app, Edits. The app is
set to...
1 week ago
No comments:
Post a Comment