Friday, December 12, 2008

Mahakama Nigeria yakataa uchaguzi kurudiwa

Mahakama Kuu ya Nigeria imekataa pingamizi la mwisho kuhusiana na uchaguzi mkuu wa rais wa mwaka jana uliompa ushindi rais wa sasa Umaru Yar'Adua.

Viongozi wa upinzani wameitaka mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi kwa maelezo uchaguzi huo ulitawaliwa na ghasia na wizi wa kura.

Waangalizi wa ndani na wa kimataifa walioshuhudia uchaguzi huo pia walishutumu namna uchaguzi huo wa mwezi wa Aprili mwaka jana ulivyoendeshwa.

Lakini Mahakama Kuu imekataa pingamizi hilo lililokubaliwa na mahakama za chini kwa madai kuwa mawakili hawakutoa ushahidi wa kutosha kuweza kutengua matokeo hayo.

Kwa maana hiyo kwa mujibu wa Jaji Niki Tobi wa mahakama kuu, mahakama hiyo imemthibitisha, Umaru Yar'Adua ndie rais na Dr Goodluck Jonathan ni makamu halali wa rais wa Nigeria.

Nigeria kwa sasa inakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi kwa sababu ya kuanguka bei ya mafuta, chanzo kikuu cha mapato ya Nigeria.

No comments:

Post a Comment