Monday, December 29, 2008

Gaza yawaka moto



Serikali ya Israel imeidhinisha kuitwa kwa wanajeshi wake wa akiba, wakati ndege za kijeshi zikiendelea kushambulia Ukanda wa Gaza.

Wanajeshi wasiopungua 6,500 wa akiba wanatarajiwa kutayarishwa.

Israel imeonya kuwa huenda ikapeleka wanajeshi Gaza, iwapo mashambulizi ya sasa ya anga yatashindwa kuzuia mashambulizi ya mabomu ya Palestina dhidi ya himaya ya Israel.

tahadhari

Katika mkutano wa baraza la mawaziri, waziri mkuu Ehud Olmert inasemekana amewatahadharisha mawaziri kuwa mapigano yatakuwa ya muda mrefu na magumu.

Mjini Gaza ndege za Israel zimeshambulia jengo kuu la usalama, ambalo ni makao makuu ya kituo cha televisheni kinachomilikiwa na Hamas, pamoja na msikiti.

Wauguzi wa Palestina wanasema zaidi ya watu 280 wameuawa tangu jana.

upungufu wa dawa

Kwa upande wa Palestina, wapiganaji wake wamerusha mabomu yaliyoelekezwa ndani zaidi ya Israel.

Wakati huohuo madaktari mjini Gaza wanasema wanajitahidi kukabiliana na idadi kubwa ya majeruhi wanaotokana na mashambulizi ya anga ya Israel.

Daktari mmoja ameiambia BBC kuwa hospitali yake ina upungufu mkubwa wa dawa na maji safi na jenereta za hospitali hiyo zinaanza kuishiwa na mafuta.


Source: BBC

No comments:

Post a Comment