Thursday, December 4, 2008

Tevez awateveza Blackburn

Carlos Tevez amempa Sir Alex Ferguson ukumbusho wa aina yake baada ya kupachika bao nne peke yake kati ya goli tano walizofunga na kuipeleka Man United katika hatua ya nusu fainali ya kombe la Carling Cup Uingereza.

Mshambuliaji huyo wa Argentina msimu huu haonekani sana dimbani kutokana na Dimitar Berbatov na Wayne Rooney kuwa chaguo la kwanza la Alex Ferguson.Alikuwa ni Tevez tena aliyemtengenezea pasi safi Nani kutimiza idadi ya magoli matano.

Kiungo wa zamani wa Man United Paul Ince, ambaye sasa ni kocha wa Blackburn alikuwa akishangaa na kushika tama baada ya kipigo hicho cha mara yake ya kwanza kwenda Old Trafford kama kocha.

Katika Matokeo mengine ya mashindano hayo ya Carling Cup timu ya Tottenham iliweza kuitolea uvivu timu ya Watford baada ya kuipa kifinyo yabisi cha bao 2-1 na kuweza kutinga moja kwa moja hatua ya nusu Fainali, kwa goli safi la pili lililofungwa kiufundi na mshambuliaji Darren Bent.

Kwa matokeo hayo Derby,Burnley,Tottenham na Man United zimefanikiwa kuingia nusu fainali na wanasubiria ratiba ya hatua hiyo ambayo inategemewa kupangwa siku ya jumamosi saa sita mchana kwa muda wa uingereza.

No comments:

Post a Comment