Thursday, December 11, 2008

Mugabe asema kipindupindu kimekwisha

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema hakuna maradhi ya kipindipindu nchini kwake huku -Umoja wa Mataifa ukionya hali inazidi kuwa mbaya.

Rais Mugabe pia amedai mataifa ya Magharibi yamepanga njama kutumia ugonjwa wa kipindupindu kama kisingizio cha kuivamia Zimbabwe na kumpindua.

Amesema hayo wakati wilaya moja inayopakana na Afrika Kusini ikitangaza eneo hilo ni la maafa kutokana na kuenea kwa maradhi hayo, ambayo yamekwishaangamiza maisha ya mamia ya Wazimbabwe.

Akihutubia taifa kwa njia ta televisheni, Bwana Mugabe amesema anafuraha kueleza kwamba madaktari wa nchi yake wakisaidiwa na wengine wameweza kuukabili ugonjwa wa kipindupindu.

No comments:

Post a Comment