Saturday, December 20, 2008

Mwalimu Misri matatani kwa kuua mwanafunzi

Mwalimu wa somo la hisabati nchini Misri ameshtakiwa akituhumiwa kumchapa hadi kumuua mwanafunzi wake wa miaka 11 kwa madai ya kutofanya kazi za shule alizompatia.

Baada ya kumchapa kwa kutumia rula mwalimu huyo, Haitham Nabeel Abdelhamid, mwenye umri wa miaka 23, inadaiwa alimtoa kijana huyo nje ya darasa na akaanza kumpiga ovyo tumboni.

Mwanaufunzi huyo Islam Amr Badr alizirai na baadae alifariki dunia hospitalini kutokana na moyo wake kushindwa kufanya kazi.

Tukio hilo lililotokea katika shule ya msingi ya Saad Othman nje ya viunga vya mji wa Alexandria mwezi wa Oktoba, limezusha tafrani kubwa nchini Misri.

Katika kesi hiyo Waziri wa Elimu anatazamiwa kuitwa mahakamani kuwa shahidi.

Baba wa mwanafunzi huyo, Amr Badr Ibrahim, amesema tatizo ni mfumo wa ufundishaji kwa vile hakuna walimu wazuri na akamshutumu Waziri wa Elimu kwa kukubali shule kuwa na walimu vijana kama huyo aliyemuua kijana wake na ametaka Waziri wa Elimu awe mshitakiwa wa kwanza.

Wamisri wengi, kesi hiyo ni kigezo cha kutisha juu ya mfumo wa elimu wa nchi yao, ambapo walimu vijana wengi hawana uzoefu na pia kutokana na uchache wao, hujikusuru kufundisha darasa moja lenye wanafunzi kati ya 60 hadi 100.


Source: BBC

No comments:

Post a Comment