Timu ya soka ya URA ya Uganda jana ilianza vyema michuano ya Kombe la Tusker baada ya kuilaza Mtibwa Sugar 1-0 katika mechi ya fungua dimba iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini, Dar es Salaam.
Bao la URA lilizamishwa na Tony Maweje katika dakika ya 50, ambaye alipokea pasi kutoka kwa Eric Obua katika mchezo huo wa kundi A.
Leo mashindano hayo yanatazamiwa kuendelea kwa kuzikutanisha Tusker FC ya Kenya na Prisons ya Tanzania.
Msisimko wa mashindano hayo unatazamiwa kuanza kesho kwa pambano kati ya bingwa mtetezi, Yanga itakayovaana na URA.
What do you want to see on blogs managed by Nigerians?
-
This post was originally published on Oct 13, 2008 Its been a while now
that have been subscribing to different categories of blogs online and all
have rea...
1 month ago
No comments:
Post a Comment