Friday, December 12, 2008

Okocha: Aboutrika ni Afrika No 1

Nahodha wa zamani wa Nigeria Austin 'Jay Jay' Okocha amesema mshambuliaji Mohamed Aboutrika wa Al Ahly anastahili kupewa taji la mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka huu.

Aboutrika ni miongoni mwa wachezaji watano waliotajwa na CAF kugombania tunzo hiyo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa bara la Afrika. Wachezaji wengine waliotajwa ni Micheal Essien (Chelsea na Ghana), Didier Drogba (Chelsea na Ivory Coast), Amr Zaki (Zamalek/Wigan na Egypt) na Emmanuel Adebayor (Arsenal na Togo).

Okocha alipokuwa akihojiwa na television amefichua kwamba kwa hali yoyote kura yake itaenda kwa Aboutrika kutokana na mafanikio yake ndani ya Egypt na Ahly mwaka huu.

Okocha alisema "Aboutrika amefanya vizuri ndani ya Egypt, ameshinda kombe la mataifa ya Afrika lililofanyika Ghana, na pia ameisadia Ahly kushinda klabu bingwa ya Afrika kwa rekodi ya mara sita,"

"Amekuwa akicheza ndani ya Egypt wakati tuna maelfu ya wachezaji wengine wa Afrika wanaocheza Ulaya lakini thamani yake inaonekana zaidi kwa jinsi alivyofikia kwenye mafanikio."

Ameongeza "Amr Zaki pia amefanya vizuri mwaka huu. Ameshinda kombe la mataifa ya Afrika lililofanyika Ghana na ameonesha kiwango kikubwa kwenye ligi kuu ya Uingereza akiwa na timu yake ya Wigan.

"Wachezaji wengine kama Emmanuel Adebayor na Didier Drogba wanastahili kutajwa kwenye tunzo hiyo kwa sababu ya kile walichokifanya kwenye klabu zao za Uingereza."

Mchezaji wa mwisho kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika ijapokuwa alikuwa akicheza kwenye klabu ya nchi yake ya nyumbani alikuwa ni Mohamed Timoumi wa Morroco mwaka 1985.

Senegal itakuwa mwenyeji wa tunzo hiyo ya CAF itakayofanyika January 23.

1 comment:

  1. Nakubaliana na Okocha kuhusu Aboutrika. Jamaa ni 'mbaya', ana kila kitu cha kumwezesha kuwa mchezaji bora kabisa wa Afrika.

    ReplyDelete