Mtoto huyo wa darasa la tatu alikuwa mkazi wa Kijiji cha Gunihuna kilicho katika Kata ya Iponya wilayani Bukombe. Hilo ni tukio la pili wilayani humu kwa mtoto albino kuuawa tangu mauaji hayo ya kikatili yanayohusishwa na imani za uchawi yaanze Kanda ya Ziwa.
Tukio hilo limetokea siku chache baada ya jeshi hilo kuwakamata polisi wanne ambao wanatuhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa wauaji wa albino na kuwaachia huru.
Mwanafunzi huyo albino aliuawa juzi majira ya saa 6:00 wakati akiwa anarudi nyumbani na wenzake. Walikuwa wakitoka kuangalia video.
Habari zilizothibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga zinasema kuwa wakati mwanafunzi huyo anarudi nyumbani na wenzake hao, walikutana na wauaji hao ambao walifunika nyuso zao kwa vitambaa.
"Yullakini juhuzi za we mtoto alipowaona akaanza kulia, wakamkamata wakamuua kwa mapanga, wakachukua mikono na miguu yote na kutoweka nayo," mkuu wa wilaya ya Bukombe, Magesa Mulongo alieleza.
Alisema baada ya tukio hilo wanakijiji waliuchukua mwili wa mtoto huyo na kuupeleka nyumbani kwa mama yake ambaye ni mlemavu kwa ajili ya maandalizi ya mazishi yaliyotarajiwa kufanyika jana baada ya taratibu za kipolisi kumalizika jana.
Kwa mujibu wa Mulongo, baada ya tukio hilo watoto aliokuwa nao albino huyo walikimbia, wakaenda kutoa taarifa kwa wanakijiji jirani,
anakijiji hao hawakufanikiwa kuwakamata watu hao.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba mpaka sasa watoto watano waliokuwa na albino huyo wameshikiliwa na jeshi la polisi wilayani Bukombe kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Miguu miwili ya albino imekamatwa kwa mganga wa jadi ambaye alilimbia kabla polisi hawajamfikia.
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi hilo linafanya msako mkali mkoani humo.
Tukio la kuuawa kwa albino wilayani Bukombe ni la pili tangu mauaji hayo yaanze katika Kanda ya Ziwa.
Wakati mauji hayo yakifanyika Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, limewahoji askari polisi wanne ambao walikuwa wakifanya operesheni ya wauaji wa albino ambao wametuhumiwa kuchukua pesa kwa wauaji na kuwaachia huru.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Shaibu polisi hao watatu wametoka kituo cha polisi cha Kahama na mmoja ametoka Shinyanga na walikuwa kwenye operesheni hiyo wilayani Kahama.
Inadaiwa polisi hao waliwakamata watuhumiwa mbalimbali wa mauaji ya albino, lakini waliwaachia huru baada ya kupewa pesa.
No comments:
Post a Comment