Saturday, December 27, 2008

Ratiba ya CHAN yatoka, Tanzania yapangwa kundi A


Katika ratiba hiyo inaonesha wenyeji Ivory Coast watafungua dimba kwenye michuano hiyo ya mwanzo
ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kwa kupambana na Zambia mjini Abidjan siku ya tarehe 22 Februari.

Timu hizo ambazo zipo kwenye kundi A zimepangwa kwenye ufunguzi wa mashindano hayo utakaofanyika kwenye mji mkuu wa Ivory Coast mjini Abidjan.

Timu nyengine ambazo zimo kwenye kundi hilo la A ambalo mechi zake zitakuwa kwenye mji huo wa Abidjan ni Senegal na Tanzania.

Kundi B litakuwa na timu za Ghana, Zimbabwe, Libya na DR Congo.

Kundi hili la B mechi zake zitafanyika kwenye mji wa Bouake ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Ivory Coast.


CHAN ni mashindano mapya yalioanzishwa na CAF kwa ajili ya wachezaji wanaocheza soka kwenye nchi zao tu.

No comments:

Post a Comment