Hali ya mashaka imetanda katika mji wa Guidiguidi kaskazini mwa Cameroon ,baada ya viungo vya siri vya wanaume kupotea muda mfupi tu baada ya kupeana mkono.
Hali hiyo ya mashaka imetanda kwa wanaume wa mji huo baada ya wanaume watatu kujitokeza wakidai viungo vyao vya siri vimeyeyuka katika mazingira ya kutatanisha baada ya kupeana mikono na mwanaume mwingine waliyemhisi ameiba viungo vyao vya siri.
Mwanaume huyo alivamiwa na kupigwa vibaya na wananchi wenye hasira, hata hivyo wanaume watatu waliodai wamepoteza viungo vyao walikimbizwa hospital ambapo baada ya vipimo kadhaa hakukuonekana upungufu wowote katika maumbile yao.
Wanaume wengine katika miji ya Maga na Puse nao walidai kupotea kwa viungo vyao vya siri ingawa vipimo vya hospitali havikuthibisha madai hayo.
Katika hali ya kutatanisha wanaume sita waliangua kilio hadharani wakidai kupotea kwa viungo vya siri baada ya kusalimiana kwa mikono na mwanaume mwingine wasiyemfahamu.
Madai hayo yalisababisha vurugu na wananchi kumvamia mshukiwa na kuanza kumpiga wakidai awarudishie viungo vyao vya siri alivyoviiba.
Polisi waliwahi kumuokoa mshukiwa na kuwachukua wanaume waliosema wamepoteza viungo vyao kwenda kuwapima. Hata hivyo madai yao pia hayakuweza kuthibtishwa.
Mmoja wa wanaume hao alisema alizubaishwa na salamu za jamaa waliyemshuku na anahisi viungo vyake vya siri vimeingia tumboni.
Introducing Celebration E-Cards: Your Digital Connection Hub
-
We are excited to introduce to you, Celebration E-Cards—an ecards online
platform designed to bridge the gap between heartfelt celebrations and the
ease of...
5 weeks ago
No comments:
Post a Comment