Tangazo
Tunapenda kuwakumbusha na kuwapa nasaha ya kufunga siku ya 'Arafah ambayo itakuwa siku ya Jumapili (07.12.2008 M) Inshaa-Allaah.
Fadhila yake ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili; uliopita na tulionao. Kadhalika tusisahau kuifufua Sunnah iliyosahauliwa ya kuleta Takbiyratul Muqayyad ambayo ni Takbiyrah inayotakiwa kusomwa kila baada ya Swalah za fardhi kuanzia siku ya 'Arafah baada ya Swalaatul-Fajr hadi mwisho wa Ayyaamut-Tashriyq (Yaani tarehe 13 Dhul-Hijjah) baada ya Swalaatul-'Asr ndio kumalizika kwake.
Kufanya hivyo hakuchukui hata dakika 2. Na inapasa kuwakumbusha ndugu wengine ili kila mmoja apate thawabu za kuifufua Sunnah hii ambayo wengi wameiacha.
Thawabu hizo zitazidi kuongozeka kwa yule atakayeanza kumfundisha mwenziwe na ataendelea kuchuma thawabu tele kila mafunzo hayo yatakapoendelea kufundishwa: Anasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((من سن في الإسلام سنة حسنة كان له أجرها وأجر من
عمل بها من بعده لا ينقص ذلك من أجورهم شيئاً ... ))
أخرجه مسلم في صحيحه
((Atakayefanya kitendo chema katika Uislam atapata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao chochote…)) [Muslim]
Inavyopasa kufanya Takbiyrah baada ya kutoa salaam ni hivi:
الله أكبر. الله أكبر. لا إله إلا الله. والله أكبر. الله أكبر ولله الحمد
"Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Laa Ilaha Illa Allaah Wa-Allaahu Akbar, Allaahu Akbar Walillahil-hamd
Sikiliza Takbiyrah Za 'Iyd
No comments:
Post a Comment