Mazishi yamefanyika huku viongozi waliofanya mapinduzi wakijitahidi kutafuta kutambulika kimataifa.
Jeneza la Bw. Conte lilipelekwa katika bunge la nchi hiyo, ambapo marais kadhaa wakiwemo wa Sierra Leone, Liberia, Ivory Coast, Guinea Bissau na wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika wamehudhuria sala maalum.
Hata hivyo kiongozi wa mapinduzi Kapteni Camara hakuonekana.
Wakati huohuo, serikali ya Ufaransa imewataka viongozi wapya nchini Guinea kuandaa uchaguzi ulio huru na wa haki katika kipinddi cha miezi 6, na sio ifikapo mwisho wa mwaka 2010, kama alivyosema kiongozi wa mapnduzi, Kapteni Camara.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Ufaransa mjini Paris amesema wananchi wa Guinea wanatakiwa kuwa huru kuchagua wanayemtaka.
Msemaji huyo amesema Ufaransa, ambayo kwa sasa inashikilia urais wa Umoja wa Ulaya, itawakilishwa katika mkutano na viongozi wa mapinduzi mjini Conakry Jumamosi.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment