MWANAMUZIKI Joseph Antonio Cartagena ‘Fat Joe’ amesema Afrika ni moja kati ya sehemu alizopenda kuja kufanya onyesho na kuweka wazi hisia zake kwa mabinti wa bara hili.
Fat Joe alisema amewaona wasichana wengi wa Afrika kuwa ni wazuri kimwonekano kuliko wengi walioko barani Amerika na Ulaya.
Akizungumza mapema wiki hii wakati wa onyesho lake katika tamasha la Klimax lililofanyika katika viwanja vya Leaders, Fat Joe alisema wakati anafanya mipango ya kuja Afrika, rafiki yake mmoja alimueleza mambo mbalimbali kuhusu Afrika lakini ni tofauti na kile alichokiona tangu alipowasili Tanzania.
“Rafiki alinieleza mengi kuhusu Afrika na kunitaka nisije huku.., lakini hali ni tofauti kabisa, watu wakarimu, nimeona mabinti wengi wazuri na wanaovutia…naweza kutamka kuwa namtaka mmoja aliye mpweke,” alisema Fat Joe.
Fat Joe alitumbuiza sambamba na Eve E na kundi la R&B la kutoka Nigeria, P Square.
Introducing Celebration E-Cards: Your Digital Connection Hub
-
We are excited to introduce to you, Celebration E-Cards—an ecards online
platform designed to bridge the gap between heartfelt celebrations and the
ease of...
5 weeks ago
No comments:
Post a Comment