Sunday, December 14, 2008

Mrembo wa Russia atwaa taji la Miss World

Miss world 2008 Kseniya Sukhinova kutoka Russia.


MWAKILISHI wa Tanzania katika shindano la Miss World, Nasreen Karim, jana aliambulia patupu katika shindano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Sanditon Convention Centre, Johannesburg, Afrika Kusini, huku mrembo wa Russia, Kseniya Sukinova, akiibuka mshindi.

Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo, Julia Morley, nafasi ya pili, ilikwenda kwa mrembo wa India, Omana Cottan, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Gabrielle Walco wa Trinidad& Tobago.

Baada ya kwisha kwa shindano hilo, mshindi alivishwa taji na mrembo Zilling Zhan wa China aliyemaliza muda wake.

Warembo wengine waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora, ni Brigitte Santos wa Angola na Tasey Coetzef wa Afrika Kusini.

Shindano hilo lililoshindanisha wanyange 100, mrembo wa Tanzania, Nasreen alipanda jukwaani akiwa amekosa mataji ya awali katika shindano hilo la 58 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1950.

Mataji ya awali ambayo Nasreen alifanya vibaya ni kipaji, bikini na michezo, hivyo jana alipanda jukwaani akiwa na matumaini finyu ya kufanya vema.

Kushindwa kwa Nasreen, ni mwendelezo wa Tanzania kuzidi kufanya vibaya tangu mwaka 1994.

Aina Maeda (1994), Emily Adolf (1995), Shose Senare (1996), Saida Kessy (1997), Basila Mwanukuzi (1998), Hoyce Temu (1999) na Jacqueline Ntuyabaliwe (2000).

Wengine ni Happiness Magese (2001), Angela Damas (2002), Sylvia Bahame (2003), Faraja Kota (2004), Namcy Sumary (2005) aliyeambulia Miss World Afrika, Wema Sepetu (2006) na Richa Adhia mwaka 2007.

Nafasi ya pili ilishikiliwa na mrembo Parvathy Omanakuttan kutoka India.


Mrembo Gabrielle Walcott kutokaTrinidad and Tobago alishika nafasi ya tatu.


Mrembo Brigite Santos kutoka Angola aliingia kwenye tano bora.


Mrembo Tansey Coetzee kutoka South Africa naye aliingia kwenye tano bora.

No comments:

Post a Comment