Thursday, December 11, 2008

Juande Ramos aanza vizuri Real Madrid

Kocha mpya wa Real Madrid ameanza vyema kazi yake ya ukocha ndani ya klabu hiyo baada ya timu yake kuikandamiza timu ya Zenit St Petersburg kwa jumla ya mabao matatu kwa bila.

Kocha huyo amechukua nafasi ya Bernd Schuster aliyefukuzwa kazi ya ukocha baada ya timu hiyo kuwa na matokeo mabaya katika siku za hivi karibuni.

Ikumbukwe kwamba msimu wa ligi ya Russia umeshamalizika jambo lililopelekea vijana hao Russia wanaofundishwa na kocha Dick Advoocat kuonekana dhahiri kwamba hawakuwa fiti na kusababisha Real madrid kuutawala zaidi mchezo huo.

Madrid waliandika bao lao kwanza kupitia kwa Raul kwenye dakika ya 25 kabla Arjen Robben hajaongeza bao la pili katika dakika ya 50, goli la tatu lilihitimishwa tena na Raul ambaye ameweza kumpita Filippo Inzaghi kwa goli moja zaidi ambaye alikuwa akiongoza kwa kuwa na magoli mengi kwenye michezo hiyo ya klabu bingwa ya Ulaya.

Matokeo mengine ya mechi hizo za klabu bingwa ya Ulaya yalikuwa kama ifuatavyo:

Group E
Celtic 2-0 Villarreal
Manchester U. 2-2 Aalborg BK


Group F
Lyon 2-3 Bayern Munich
Steaua Bucurest 0-1 Fiorentina

Group G
Dynamo Kyiv 1-0 Fenerbahce
FC Porto 2-0 Arsenal

Group H
Juventus 0-0 BATE Borisov

No comments:

Post a Comment