Friday, December 19, 2008

Ratiba ya ligi ya mabingwa wa ulaya yatolewa














Kwa mujibu wa ratiba ya mechi za timu 16 bora iliyotangazwa leo, Mabingwa wa soka uingereza Man United itakuwa na kibarua kigumu cha kufunga safari ya moja kwa moja hadi San Siro kuwakabili Mabingwa wa soka Italia Timu ya Inter Milan katika hatua ya 16 bora ya mabingwa ulaya.


Wakati timu ya Liverpool wao watakua na safari fupi lakini yenye ugumu wa aina yake pale watakapotua katika jiji la Madrid kuivaa uso kwa uso Real Madrid.

Nae kocha wa zamani wa Chelsea Claudio Ranieri akiwa na ndoto yake ya siku nyingi ya kurejea Stamford Bridge, hatimaye ndoto hiyo imetimia na ataiongoza Juventus kwenda kuminyana mbavu na vidume vya London Chelsea.

Wajukuu wa Arsene Wenger watajiweka tayari ndani ya uwanja wa Emirates kuisubiri timu ya As Roma timu yenye mazoea ya kwenda uingereza mara kwa mara katika mashindano hayo.

Mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa kati ya tarehe 24/25 Februari na 10/11 machi .

Ratiba kamili ya mechi hizo ni kama ifuatavyo:
Chelsea Vs Juventus
Villarreal Vs Panathinaikos
Sporting Lisborn Vs Bayern Munich
Atletico Madrid Vs Fc Porto
Lyon Vs Fc Barcelona
Real Madrid Vs Liverpool
Arsenal Vs As Roma
Inter Milan Vs Man United

No comments:

Post a Comment