Friday, January 30, 2009

Walimu Kenya warudi darasani

Maelfu ya walimu nchini Kenya wamerudi kazini baada ya mgomo wao uliodumu kwa zaidi ya wiki moja kuvunjwa kufuatia makubaliano na serikali.

Kulingana na Katibu Mkuu wa chama cha walimu, KNUT, Lawrence Majali chama hicho kimekubali kufanya mkataba mpya na serikali kuhusu malipo ya nyongeza ya walimu.

Mgomo huo ulikuwa umeitishwa baada ya serikali kusema haingeweza kuafikiana na matakwa ya walimu ya kutaka nyongeza kubwa ya mishahara kwa mpigo.

Wizara ya Elimu inatakiwa kulipa jumla ya dola milioni 96 kama nyongeza kwa walimu zaidi ya laki mbili.

Katibu Mkuu Majali amesema sasa walimu watalipwa kwa awamu mbili.

Kuanzia mwezi Julai mwaka huu watalipwa asilimia arobaini na masalia kulipwa Julai mwaka ujao.


Source: BBC

No comments:

Post a Comment