Monday, January 19, 2009

Ukubwa wa uharibifu Gaza waonekana

Wanajeshi wa Israel wakiondoka Gaza

Ukubwa wa uharibifu kufuatia mashambulio ya wiki tatu ya Israel huko Gaza, sasa umeweza kuonekana baada ya pande zote mbili Israel na Hamas kutangaza kusimamisha mapigano.

Afisa wa Umoja wa Mataifa John Ging amesema watu nusu milioni hawana maji tangu mzozo huo ulipoanza na wengine wengi hawana umeme.

Nyumba elfu nne zimeharibiwa kabisa na kubakia magofu na maelfu ya watu hawana makazi.

Msemaji wa serikali ya Israel Mark Regev amesema ana matumaini mpaka kwa ajili ya kupitishia misaada utafunguliwa baadae leo.

Waziri Mkuu wa Israeli Ehud Olmert amesema anataka majeshi ya nchi yake kuondoka haraka iwezekanavyo na baadhi wameshaondoka.

Israel ilitangaza kusimamisha mapigano siku ya Jumamosi na ikajigamba imefikia malengo yake ya kivita.

Baadae Hamas ilitangaza mpango wake wa kuacha mapigano huku mmoja wa viongozi wake akidai "wamepata ushindi" dhidi ya Israel.


Source: BBC

No comments:

Post a Comment