Watu wanaodaiwa kuwa ni wenye hasira kali wamewaua kwa kuwachoma moto watu watatu katika kijiji cha Kidahwe kata ya matendo mkoani Kigoma baada ya kuwabaini wakifanya jaribio la kupora baiskeli
Kwa mjibu wa kamanda wa polisi mkoani Kigoma Abdihak Rashid tukio hilo la kuuawa kwa watu hao lilitokea siku ya ijumaa january 16 majira ya saa 11 jioni ambapo watu hao watatu waliouawa wakiwa na mapanga na nondo walimvamia Bw.Cassiano ambaye ni mkazi wa kijiji hicho kwa lengo la kumnyang'anya baiskeli yake
Kamanda Rashid aliongeza kuwa mara baada ya Bw.Cassim kupiga kelele za kuomba msaada ndipo wananchi wema walijitokeza kutoa msaada na kuanza kupambana na watu hao ambao walizidiwa nguvu na kupigwa hadi kufa na kisha kuchomwa moto kwa hasira
Hadi sasa miili ya watu hao haijatambuliwa kwa majina na imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa Maweni wakati gwaride la utambulisho likiendelea toka kwa watu ambao wanaweza kuwa ndugu zao
Aidha kamanda Abdhaki amekemea tabia hiyo ya wananchi kujichulia madaraka mikononi na kuwataka kuwa na utamaduni wa kufuata sheria wanapowabaini watuhumiwa kwani ni ruksa kwa mtu yeyote kujichukulia madaraka kutoa maisha ya mwingine
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa hatua hiyo imefikiwa na wananchi hao kufuatia kuchoshwa na matukio ya mara kwa mara ya ujambazi hivyo wanapombaini mtu yeyote kujihusisha na vitendo hivyo wanajikuta wameua bila kukusudia.
No comments:
Post a Comment