Friday, January 23, 2009

Bi Clinton aanza wadhifa wake rasmi leo

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Hillary Clinton

Wafanyakazi katika idara ya mashauri ya kigeni ya Marekani wamempokea kwa furaha Bi. Hillary Clinton ambaye ameanza rasmi kazi yake hii leo katika wizara hiyo.

Akipokewa kwa shangwe na nderemo, Bi Clinton amesema hii ni enzi mpya kwa Marekani. Akiongezea kusema kuwa atahakikisha kuwa diplomasia na maendeleo zinatumika kama vyombo muhimu vya kuimarisha siku za baadae za Marekani.

Alionya kuwa kazi inayowakabili sio rahisi.Nao wafanyakazi katika idara hiyo kwa upande wao wamesema wako tayari kufanyakazi na Bi Clinton na kumsaidia katika kuyafikia malengo yake makubwa .

Utawala wa Rais Obama tayari umeanza kushughulikia masuala kadhaa ya sera za kigeni na usalama ambapo leo Rais Obama ametia saini maagizo ya kufunga gereza la Guatanamo Bay katika pindi cha mwaka mmoja.


Source: BBC

No comments:

Post a Comment