Tuesday, January 13, 2009

Gesi yaanza kusambazwa tena Ulaya

Mitambo ya gas ya Urusi na Ukraine

Saa chache baada ya kutangaza kwamba imerejesha usambazaji wa gesi, kampuni kubwa ya gesi ya Urusi Gazprom sasa imeilaumu Ukraine kwa kufungia bidhaa hiyo kuingia barani Ulaya.

Ukraine Kwa upande wake imesema Urusi imebadilisha njia ya kusambazia gesi hiyo bila kuijulisha mabadiliko hayo.

Urusi ilisimamisha usambazaji wa gesi hiyo wiki moja iliyopita baada ya kuilaumu Ukraine kuiba bidhaa hiyo ikiwa njiani Ulaya.


Source: BBC

No comments:

Post a Comment