Saturday, January 3, 2009

Sheria 'utata' yapitishwa Kenya


Rais wa Kenya, Mwai Kibaki ametia saini muswada wa marekebisho ya sheria ya mawasiliano ya mwaka 2008, licha ya pingamizi kutoka kwa wadau wa sekta ya habari nchini humo.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, rais Kibaki amesema udhibiti wa vyombo vya habari vya elektroniki (Radio na Televisheni), utasaidia kulinda utamaduni, tabia njema na utaifa.

Vyombo vya habari vinapinga muswada huo, ambao una vipengele kadhaa, moja wapo kikiwa kimoja kinachompa nguvu waziri wa Usalama wa nchi kuvamia vyombo vya habari na pia kunyanganya vifaa vya utangazaji.


Source: BBC

No comments:

Post a Comment