Rapa na mwimbaji nguli wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars `Twanga Pepeta International`, Khalid Chuma `Chokoraa`, ameanza mwaka mpya wa 2009 vibaya, kwa kumwaga damu ukumbini.
Chokoraa alimwaga damu juzi usiku wakati Twanga Pepeta ilipokuwa ikitumbuiza katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya 2009 kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha.
Twanga ilitua Arusha baada ya mkesha wa mwaka mpya kupagawisha mashabiki kwenye hoteli ya Safari Park jijini Nairobi, Kenya.
Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kurejea kutoka Arusha, Chokoraa alisema aliumia vibaya na kupasuka chini ya kidevu, akang`oka meno mawili na pia kupata maumivu sehemu za kifua baada ya kuteleza na kuanguka vibaya.
``Mwaka 2009 nimeuanza vibaya kwa kumwaga damu, Januari mosi majira ya saa sita usiku kwenye shoo ya kufungua mwaka Arusha, katika mishemishe za kupagawisha mashabiki nilikuwa nacheza shoo, nikatelekeza, nikafikia kifua na kidevu, nikachanika na meno mawili kung`oka,`` alisema Chokoraa.
Twanga Pepeta ilitarajiwa kurejea nchini jana na leo kutarajia kuwachengua mashabiki kwa staili zake mpya za `Sugua Kisigino` ya Saulo John `Ferguson`, `Nimeokota Kidude` ya Chokoraa na Weka Selo, Kitumbua mbona wauza usiku, Obama, Wizi Mtupu na Mambo Maregea za Msafiri Said `Diouf`.
Source: Nipashe
Meta Unveils Edits: A Video Editing App for Creators
-
Meta, the parent company of Facebook and Instagram, is making waves once
again with the announcement of its new video editing app, Edits. The app is
set to...
1 week ago
No comments:
Post a Comment