Wednesday, January 28, 2009

Machafuko yazuka kisiwani Madagascar

Ghasia zimeendelea kukumba mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo, kufuatia maandamano dhidi ya serikali ambapo zaidi ya watu 20 wameuawa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Antananarivo, waliouawa huenda walikuwa watu waliokuwa wakipora mali wakati wa maandamano hayo.

Iliwalazimu polisi kupiga risasi hewani ili kutawanya umati mkubwa wa waandamanaji na waporaji.

Hii ni siku ya nne tangu ghasia kuzuka nchini humo kufuatia mzozo kati ya meya wa mji huo na rais.

Wazima moto walipata miili hiyo 20 katika duka moja ambalo lilikuwa limeteketea.

"Ninaweza kuthibitisha kwamba tulipata miili 25. Ilikuwa imechomeka zaidi na itakuwa vigumu kuitambua," alisema afisa mmoja mkuu wa idara ya wazima moto.

Meya wa upinzani wa Antananarivo na Rais Marc Ravalomanana wametoa wito wa kuwepo na utulivu.


Source: BBC

No comments:

Post a Comment