Sunday, February 15, 2009

Zimbabwe bado yazongwa na mizengwe

Bw Bennet ni mwanasiasa aliyewahi kuwa mkulima

Polisi nchini Zimbabwe wamemfungulia mashtaka ya uhaini mwanachama mwandamizi wa chama cha MDC kinachoongozwa na waziri mkuu Morgan Tsvangirai, chama hicho kimeeleza.

Roy Bennett, mteuliwa wa kiti cha naibu waziri wa kilimo, alifunguliwa mashtaka saa chache baada ya kuapishwa kwa baraza jipya la mawaziri kwa mujibu wa mkataba wa kugawana madaraka, chama cha MDC kimeeleza.

Taarifa ya chama hicho imeelezea mashtaka hayo kuwa ni kashfa na yenye mwelekeo wa kuchochewa kisiasa.

Awali, sherehe ya kuapishwa kwa baraza hilo ilikumbwa na utata kuhusu mgawanyo wa viti vya mawaziri.

Kwa mujibu wa mkataba wa ugawanaji madaraka ulioafikiwa baada ya miezi mingi ya majadiliano tangu uchaguzi uliozua mzozo, chama cha Zanu-PF kinachoongozwa na rais Robert Mugabe kitapata viti 15 na makundi mawili ya MDC yanayopingana yatagawana viti 16 serikalini.

Lakini wanachama saba zaidi wa Zanu-PF walijitokeza ikulu mjini Harare kuapishwa.Swala hilo lilipatiwa ufumbuzi baada ya majadiliano makali yaliyofanyika kwa faragha.


Source: BBC

No comments:

Post a Comment