Thursday, February 19, 2009

Mahakama maalum Kenya yaahirishwa

Mahakama maalum kuwashtaki walioshiriki ghasia baada ya uchaguzi yaahirishwa Kenya

Waziri Mkuu wa Kenya amesema nchi hiyo inayo miezi miwili kusubiri kabla ya kuanzishwa mahakama maalum ya kuwashtaki waliohusika na ghasia baada ya uchaguzi.

Bwana Raila Odinga amesema Kofi Annan ameafiki kusogezwa mbele muda wa kuanzishwa mahakama hiyo.

Bwana Annan alisimamia upatanishi hadi kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa mwaka mmoja uliopita, hali iliyomaliza ghasia ambapo watu takriban 1,500 waliuawa.

Wiki iliyopita wabunge waliukataa muswada wa kuundwa mahakama hiyo, licha ya juhudi za ushawishi kutoka kwa Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu, Mr Odinga.

Wanaoupinga muswada huo walisema hawana imani na mfumo wa sheria wa Kenya na wametaka watuhumiwa wote ni lazima wafikishwe mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya The Hague- ICC.



Source: BBC

No comments:

Post a Comment