Monday, February 23, 2009

Stars Yalala, Zambia Yaua

Mchezaji wa Senegal, Mamadou Traore (kushoto) akigombea mpira na kiungo wa Tanzania, Geoffrey Bonny Namwandu (kulia) katika mchezo wa Kombe la CHAN uliochezwa uwanja wa Felix Houphouet-Boigny mjini Abidjan, Ivory Coast. Stars ilala 1-0.


TANZANIA kwa mara nyingine imeanza vibaya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN, baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Senegal, huku jirani zao Zambia wakitoa onyo kwa timu nyingine kwa kuwafunga wenyeji wa michuano hiyo ya CHAN, Ivory Coast kwa mabao 3-0.



Taifa Stars iliyoanza mchezo huo vibaya kwa safu ya ulinzi kushindwa kuelewana vizuri na kuacha mipira ya juu kutawaliwa na washambuliaji wa Senegal waliokuwa makini zaidi kutumia mwanya huo.



Mshambuliaji Mamadou Traore aliunganisha vizuri krosi kwa kichwa kilichomshinda kipa Shabaan Dihile katika dakika ya 29 na kuipa Ivory Coast bao pekee.



Kuingia kwa bao hilo kulirudisha hali Stars kujaribu kufanya mashambulizi mengi kupitia kwa winga wake Mrisho Ngassa aliyekuwa chini ya ulinzi mkali wa ngome ya Senegal.



Kocha Marcio Maximo alijaribu kuwatoa Godfrey Bonny, Haruna Moshi na Jerry Tegete walioshindwa kuonyesha kiwango cha kuvutia na nafasi zao kuchuliwa na Nurdin Bakari, Musa Hassan Mgosi na Abdi Kassim.



Kuingia kwa wachezaji hao Taifa Stars ilichangamka na kufanya mashumbulizi mengi katika kipindi cha pili, lakini walishindwa kumalizia nafasi nyingi walizotengeneza.



Katika mchezo wa awali kati ya wenyeji wa michuano hiyo ya Afrika, Ivory Coast walipokea kipigo kitakatifu cha mabao 3-0 kutoka kwa Zambia 'Chipolopolo'.



Mshambuliaji Given Singuluma ndiye aliyekuwa shujaa wa mchezo huo kwa kufunga mabao yote matatu ya Zambia katika dakika ya 36,47 na 76, na kuharibu sherehe zote za ufunguzi mbele ya rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast.




Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment