Monday, February 23, 2009

Kambi ya AU yashambuliwa Mogadishu

Burundi na Uganda ndizo pekee zina wanajeshi Mogadishu


Waasi nchini Somalia wameshambulia kambi ya jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika mjini Mogadishu.

Kundi la wanamgambo wa kiislamu la al-Shabab limesema kuwa wafuasi wake wawili walifanya shambulio la kujitolea muhanga kwa kutumia gari.

Jeshi la AU limesema linafanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo lakini halikutoa idadi ya wanajeshi waliojeruhiwa au kuuawa.
Msemaji wa wanajeshi kutoka Burundi, ambayo inachangia walinda amani katika jeshi hilo amesema wanajeshi wao sita waliuawa katika tukio hilo, shirika la habari la AFP limearifu.

Jumla ya wanajeshi 3,500 wa kulinda amani kutoka Burundi na Uganda ndiyo pekee wa kigeni walioko Mogadishu tangu mwezi Januari wakati majeshi ya Ethiopia yaliyokuwa yakiiunga mkono serikali yalipoondoka.

Makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa kati ya serikali ya mpito ya Somalia na kundi la upinzani lenye msimamo wa kadri, yalitoa fursa kwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed kuchaguliwa kuwa rais mpya mwezi Januari, lakini kundi la al-Shabab limeapa kuendeleza mapambano ya silaha dhidi ya wanajeshi wa kulinda amani.



Source: BBC

No comments:

Post a Comment