Timu ya taifa, Taifa Stars, jana iliaga kiume fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani, CHAN, baada ya kubakiza dakika mbili tu kuingia nusu fainali.
Stars iliyohitaji kushinda, ama kupata sare lakini Segegal ifungwe angalau bao moja zaidi yake na wenyeji Ivory Coast ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 86.
Mrisho Ngassa aliyekuwa akielekea golini aliangushwa ndani ya eneo la hatari na Shadrack Nsajigwa akafunga kwa penalti.
Lakini Zambia ambayo ilikuwa itolewe kwa ushindi wa Stars ilicharuka na kufunga katika dakika ya nne ya muda wa nyongeza wa dakika sita zilizochezwa, kutokana na mpira wa kona.
Mchezo kati ya Ivory Coast na Senegal iliyoongoza kundi mbele ya Zambia kwa uwiano wa mabao ulimalizika kwa suluhu.
Stars:
Shaabam Dihile, Shadrack Nsajigwa, Juma Jabu, Salum Swedi, Nadir Haroub` `Cannavaro`, Nurdin Bakari, Henry Joseph (Shabaan Nditi dk.69), Nizar Khalfan, Mussa Hassan `Mgosi`, Mrisho Ngassa na Kigi Makassy (Jerry Tegete dk.72).
Source: Lete Raha
What do you want to see on blogs managed by Nigerians?
-
This post was originally published on Oct 13, 2008 Its been a while now
that have been subscribing to different categories of blogs online and all
have rea...
1 month ago
No comments:
Post a Comment