Chama cha MDC nchini Zimbabwe kimesema kitafanya uchunguzi wake kuhusu chanzo cha ajali iliyotokea siku ya Ijumaa ambapo mke wa Morgan Tsvangirai', Bi Suzan aliuawa.
Hata hivyo maafisa wamesema hakuna jambo lolote linaloashiria kuwa kulikuwa na njama iliyosababisha ajali hiyo.
Ubalozi wa Marekani nchini Zimbabwe umesema gari la mizigo lililohusika katika ajali kwa kugongana na lile la Bw Tsvangirai, linamilikiwa na taasisi inayofanya kazi na shirika la misaada la Marekani, USAID.
Katibu mkuu wa MDC, Tendai Biti ametoa rambi rambi kwa kifo cha mke wa Bw Tsvangirai, akimwita "mama yetu sisi na mapambano yetu".
Jumamosi mchana, Bw Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 56, alitoka katika hospitali mjini Harare alikokuwa akitibiwa majeraha aliyoyapata kwenye ajali hiyo.
Ijumaa usiku alitembelewa hospitalini na mpinzani wake wa kisiasa, rais Robert Mugabe akiwa ameambatana na mkewe Bi Grace.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment