Rais Marc Ravalomanana wa Madagascar amesema kuwa yuko tayari kuruhusu kura ya maoni ifanyike kupata ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa unaoizonga nchi hiyo.
Hatua hiyo inajitokeza huku wasi wasi ukiongezeka katika mji mkuu Antananarivo, huku Bw Ravalomanana akiahidi kupuuza wito wa wanasiasa wa upinzani kumtaka ajiuzulu.
Awali wapinzani walitishia kuandamana mpaka makazi ya rais endapo Bw Ravalomanana angekataa kuachia madaraka.
Watu takriban 100 wameuawa tangu kuanza kwa maandamano mwezi Januari.
Bw Ravalomanana aliwaeleza maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika nje ya makazi yake kuwa "hatishiki" na wazo la kufanya kura ya maoni.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment