Tuesday, March 31, 2009

Dhiki ya kutafuta riziki bara Ulaya


Mamia ya wahamiaji kutoka Afrika wamefariki dunia baada ya mashua walizokuwa wakisafiria kuzama katika bahari ya Mediterranean karibu na pwani ya Libya.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia maswala ya wahamaji, IOM, huenda idadi ya watu walikufa maji ikakaribia 500.

Hadi sasa ni watu 20 peke yao ambao wameokolewa huku miili 21 ikipatikana kwenye ufuko.

Idadi kamili ya mashua walizokuwa wakisafiria haijabainika.

Tangu Mei mwaka jana Libya na Uhispania zimekuwa zikishirikiana katika kushika doria kuwadhibiti wahamiaji haramu wanaojaribu kuvuka hadi bara Ulaya.

Maafisa wa Libya wamesema mashua tatu ziling'oa nanga hapo jumapili ambapo moja ikiwa imebeba zaidi ya watu 250 ilizama.

Nchini Misri wizara ya mambo ya nje imesema maiti za raia wake 10 zimepatikana.

Kila mwaka maelfu ya Waafrika huhatarisha maisha yao wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean wakikimbilia bara Ulaya kutafuta
maisha bora.


Source: BBC

No comments:

Post a Comment