Wataalam wa afya, na viongozi kutoka barani Afrika wanahudhuria mkutano mkubwa nchini uingereza hii leo kujadili mbinu za kuzuia na kudhibiti saratani ya mlango wa kizazi au Cervical cancer barani Afrika.
Mkutano huo unatazamiwa kuibua mikakati itakayosaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya wanawake barani afrika ambao wanakumbwa saratani hiyo.
Wanawake wengi zaidi wanakumbwa na saratani ya mlango wa kizazi kuliko saratani nyingine yoyote, japo ugonjwa huu unaweza kukingwa kupitia chanjo au kutibiwa ukigunduliwa mapema.
Na utafiti uliofanywa nchini Uganda umebainisha kuwa kufanyiwa tohara huenda kukasaidia kupunguza magonjwa mengine ya zinaa mbali na Ukimwi.
Utafiti huo uliochapishwa na jarida moja la kitabibu nchini Uingereza, unasema kuwa ni nadra sana kwa wanaume waliotahiriwa kupatwa na ugonjwa wa malengelenge na virusi vya
papi-lloma, maarufu kama HPV ambavyo husababisha saratani ya mlango wa kizazi, kwa wanawake.
Utafiti wa hapo awali uliofanywa katika nchi tatu barani afrika ikiwemo Uganda, ulibainisha kuwa tohara kwa wanaume hupunguza viwango vya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa zaidi ya asilimia hamsini.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment