Saturday, March 28, 2009

Timu ya marathoni Tanzania hoi Jordan, majirani zake watamba

KAMA ilivyobashiriwa na wengi, Tanzania kwa mara nyingine imerejea mikono mitupu kutoka michuano ya kimataifa ya mbio za nyika zilizofanyika Amman, Jordan.

Tanzania ambayo iliwakilishwa na timu ya wanariadha tisa, wanaume watano na wanawake wanne iliambulia mikono mitupu, ikiziacha nchi jirani zake, Kenya, Uganda na Ethiopia zikitamba.

Michuano hiyo yenye zawadi ya fedha taslimu, dola 30,000 (Shilingi milioni 39 za Kitanzania) kwa mshindi wa kwanza hadi wa sita anayeondoka na dola 3,000 kwa upande wa mbio za wakubwa.

Pia, zawadi hizo zinatolewa kwa timu ambako ya kwanza inaondoka na dola 20,000 (Shilingi milioni 26) kwa mshindi wa kwanza ambazo zinashuka hadi dola 4,000 kwa mshindi wa sita.

Wawakilishi wa Tanzania ambao waliondoka kwa unyonge siku moja kabla ya mashindano hayo hawakuwamo katika orodha ya wakimbiaji waliomaliza mbio hizo ambazo zilikuwa zikirushwa laivu kupitia Dstv Supersport.



Source: HabariLeo

No comments:

Post a Comment