Monday, March 2, 2009

Rais wa Guinea Bissau auawa na waasi

Rais Vieira alipigwa risasi katika hatua ya kulipiza kisasi

Rais Joao Bernardo Vieira ameuawa na kundi la wanajeshi waasi ambao inaaminika walikuwa wakilipiza kisasi kufuatia mauaji ya mkuu wao wa jeshi mapema Jumatatu.

Jeshi limekanusha madai ya kufanya mapinduzi ya serikali huku hali katika mji mkuu Bissau ikiwa tulivu.

Msemaji wa jeshi Zamora Induta aliwaambia waandishi wa habari, "Rais Vieira aliuawa na jeshi wakati alikuwa akijaribu kutoroka nyumbani kwake kufuatia mashambulizi ya kundi la wanajeshi."

Zamora alimshutumu Rais Vieira kwa kuwajibu juu ya mauaji ya mkuu wa jeshi kufuatia sintofahamu kati yao.

Guinea Bissau ni moja wapo wa nchi maskini sana duniani.

Mapinduzi ya serikali si jambo geni kwa nchi hiyo ambayo pia ni maarufu kama kituo cha kupitishia mihadarati hadi bara Ulaya.



Source: BBC

No comments:

Post a Comment