Chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini, kimeshinda uchaguzi mkuu lakini matokeo ya mwisho yanaonesha chama hicho kimeshindwa kupata theluthi mbili ya wingi wa kura.
Kwa mujibu wa maofisa wa tume ya uchaguzi chama cha ANC kimezoa asilimia 65.9 kutokana na kura milioni 17, upande wa chama cha Democratic Alliance kina asilimia 16.6 ya kura huku chama cha Congress of the People (Cope) kimejipatia asilimia 7.42.
Theluthi mbili ya kura ni muhimu katika bunge kwa ajili ya kubadilisha katiba.
Matokeo hayo yanatoa nafasi kwa kiongozi wa ANC Jacob Zuma kuwa rais mpya wa Afrika Kusini wakati bunge litakapokutana.
Wafuasi wa ANC wamekuwa katika sherehe nchi nzima huku wakisubiri matokeo rasmi kutangazwa.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment