Thursday, April 2, 2009

Mkutano wa viongozi G20 waanza London

Waandamaji wakipinga ubepari

Usalama umeimarishwa jijini London wakati huu viongozi wa mataifa tajiri zaidi duniani wa kundi lijulikanalo G20 wakijiandaa kuanza mkutano wa siku moja kujaribu kuukwamua uchumi wa dunia.

Mkutano huo unalenga kukubaliana mikakati ya kudhibiti mdororo wa uchumi duniani.

Kumekuwa na dalili Ufaransa na Ujerumani kutofautiana na Marekani kuhusu mbinu za kukabiliana na tatizo hilo.

Afrika Kusini ndiyo taifa pekee barani Afrika lenye uanachama katika G20, ingawa NEPAD itawasilisha ajenda ya Afrika kwa ujumla.

Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi anahudhuria kwa nafasi yake ya mwenyekiti wa NEPAD.

Huku mkutano huo ukifanyika mashirika ya kimataifa yanatabiri uchumi wa dunia mwaka huu huenda ukadorora zaidi.

Mada ya mkutano wa G20 ni kuutafutia ufumbuzi msukosuko wa uchumi unaoikumba dunia kwa wakati huu.

Pia viongozi hao watajadili mbinu za kuzuia mdororo kama huu usitokee tena kwa siku zijazo.

Nalo Shirika la fedha duniani IMF, linapendekeza hatua za kudhibiti mfumo wa fedha duniani kupewa umuhimu.

Tofauti zimeibuka kuhusu matumizi ya pesa za umma pamoja na kupunguza kiwango cha kodi wanachotozwa watu, kama njia ya kuuchepusha uchumi.


Source: BBC




No comments:

Post a Comment