Friday, November 28, 2008

Mji wa Makkah kuweka historia duniani

Mji mtakatifu wa Waislam ‘Makkah’ uko mbioni kuboreshwa zaidi kwa kufanyiwa matengenezo yatakayoweka historia duniani.

Mojawapo ya matengenezo yatakayofanywa ni kuupanua msikiti wa sasa ujulikanao kama Al-Haram, ambao kwa sasa una uwezo wa kuchukua waumini 900,000 ambao utaongezwa kuuwezesha kuchukua waumini Millioni tatu ambao ni idadi ya waumini wanaokwenda kuhiji katika mji huo wa Mecca kila mwaka.

Matengenezo haya yataufanya msikiti huu kuwa jengo pekee duniani linaloweza kuchukua idadi hio kubwa ya watu kwa wakati mmoja.

Mipango hii ya matengenezo inasemekana inadhaminiwa na Mfalme wa Saudi Arabia Abdullah bin Abdul Aziz. Madhumuni ni kuupa sura mpya msikiti huo wenye ukubwa wa 356,800sq m. Mfalme huyo atakabidhiwa mapendekezo kutoka kwa wahandisi wa makampuni tofauti 18 mwisho wa mwezi huu.

Vyanzo vilivyoko karibu na project hii vinasema kazi hii itagawanywa katika hatua tofauti, hatua ya kwanza itauweka msikititi wa al-Haram kuingiza waumini 1.5 million. Na kuendelea hivyo mpaka kufikia millioni tatu.

Wataalam hawa pia watapewa nafasi ya kutembelea eneo hilo la msikiti wakiwa wanajaribu kupata sura ya jengo itakayo kubalika.

No comments:

Post a Comment