Aliyekua nahodha wa timu ya Arsenal William Gallas amenyang'anywa unahodha wa timu ya Arsenal na inasemekana hakusafiri na timu hiyo kwenda Manchester kwa ajili ya pambano lao la leo na Manchester City.
Sababu zilizotolewa za kunyang'anywa unahodha wa Gallas ni maneno aliyosema Gallas alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na mvutano ndani ya Arsenal.
Nafasi hiyo ya unahodha kwenye pambano la leo inaweza kushikiliwa na kipa Manuel Almunia ama mlinzi Gael Glichy.
Katika mahojiano na vyombo vya habari mwanzoni mwa wiki, Gallas alieleza kuwepo kwa kutokuelewana ndani ya timu katika mechi kadhaa ikiwemo ile ya watani wao wa jadi Tottenham waliotoka nao suluhu 4-4 mwezi uliopita.
Introducing Celebration E-Cards: Your Digital Connection Hub
-
We are excited to introduce to you, Celebration E-Cards—an ecards online
platform designed to bridge the gap between heartfelt celebrations and the
ease of...
5 weeks ago
No comments:
Post a Comment