
Kocha huyo amechukua nafasi ya Bernd Schuster aliyefukuzwa kazi ya ukocha baada ya timu hiyo kuwa na matokeo mabaya katika siku za hivi karibuni.
Ikumbukwe kwamba msimu wa ligi ya Russia umeshamalizika jambo lililopelekea vijana hao Russia wanaofundishwa na kocha Dick Advoocat kuonekana dhahiri kwamba hawakuwa fiti na kusababisha Real madrid kuutawala zaidi mchezo huo.
Madrid waliandika bao lao kwanza kupitia kwa Raul kwenye dakika ya 25 kabla Arjen Robben hajaongeza bao la pili katika dakika ya 50, goli la tatu lilihitimishwa tena na Raul ambaye ameweza kumpita Filippo Inzaghi kwa goli moja zaidi ambaye alikuwa akiongoza kwa kuwa na magoli mengi kwenye michezo hiyo ya klabu bingwa ya Ulaya.
Matokeo mengine ya mechi hizo za klabu bingwa ya Ulaya yalikuwa kama ifuatavyo:
Group E
Celtic 2-0 Villarreal
Manchester U. 2-2 Aalborg BK
Group F
Lyon 2-3 Bayern Munich
Steaua Bucurest 0-1 Fiorentina
Group G
Dynamo Kyiv 1-0 Fenerbahce
FC Porto 2-0 Arsenal
Group H
Juventus 0-0 BATE Borisov
No comments:
Post a Comment