
Fat Joe alisema amewaona wasichana wengi wa Afrika kuwa ni wazuri kimwonekano kuliko wengi walioko barani Amerika na Ulaya.
Akizungumza mapema wiki hii wakati wa onyesho lake katika tamasha la Klimax lililofanyika katika viwanja vya Leaders, Fat Joe alisema wakati anafanya mipango ya kuja Afrika, rafiki yake mmoja alimueleza mambo mbalimbali kuhusu Afrika lakini ni tofauti na kile alichokiona tangu alipowasili Tanzania.
“Rafiki alinieleza mengi kuhusu Afrika na kunitaka nisije huku.., lakini hali ni tofauti kabisa, watu wakarimu, nimeona mabinti wengi wazuri na wanaovutia…naweza kutamka kuwa namtaka mmoja aliye mpweke,” alisema Fat Joe.
Fat Joe alitumbuiza sambamba na Eve E na kundi la R&B la kutoka Nigeria, P Square.
No comments:
Post a Comment