
Hata hivyo ametoa onyo kwa Waislamu wote, kuacha kutenda vitendo viovu siku hiyo, kwani kufanya hivyo ni kuutukanisha Uislam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) jijini Dar es Salaam juzi, Mufti aliwataka Waislam nchini kusherehekea kwa utulivu na amani.
"Ni vyema Waislamu wasilewe wala kuendesha magari ovyo na kutopigana, badala yake wahudhurie misikitini kufanya dua," alisema.
Alisema kitaifa sherehe hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam na dua itafanyika katika Msikiti wa Al-Farouq ulioko Kinondoni.
Mufti alisema kuwa mgeni rasmi, bado hajafahamika.
Alisema wamepeleka maombi serikalini na kwamba wanasubiri majibu ili wajue atakayekuwa mgeni rasmi.
No comments:
Post a Comment