Sunday, January 10, 2010

Togo yajiondoa kwenye michuano ya CAF
















Mchezaji wa Togo Emmanuel Adebayor


Timu ya taifa ya Togo imejiondoa kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kufuatia kuuawa kwa dereva wa basi lao.

Wachezaji wawili wa Togo walifyatuliwa risasi na kujeruhiwa katika mkoa wa kaskazini wa Cabinda siku ya ijumaa.

Waandaaji wanasisitiza kuwa michuano itaendelea na kwamba wataimarisha usalama.

Lakini mchezaji wa Togo Alaixys Romao ameliambia gazeti moja la lugha ya kifaransa L'Equipe: "Tunazungumza na timu zengine katika kundi letu kuzishawishi zisusie."

Katika mechi yao ya kwanza siku ya Jumatatu Togo ilipangiwa kucheza na Ghana huko Cabinda na wachezaji wa timu hiyo inayojulikana kama Black Stars wamesema kuwa wako tayari kuendelea kucheza.

Ivory Coast na Burkina Faso ni timu zengine zilizopangwa katika kundi B.


Source: BBC

2 comments:

  1. Jamani kwanini umetuondolea mziki wa taarab?yani ni hudhuni kubwa kwetu wazanzibar tulioko nchi za nje kutopata tena huu mziki wa nyumbani,,samahani sana tunaomba uruhusu tuwe tuna burudika,,vipi kuhusu hii blog mbona umepotea na hakuna mapya tena?Samahani ni mmoja wa mashabiki wa hii blog.Asante.

    ReplyDelete
  2. I have been on the internet lately, looking for something to read and that is how I came across your site and saw this article of yours. So, I decided to see what it says and I find out that it is so amazing. You really did a great work in on your site and the articles you posted on it. You really take your time in posting this article or and they are clearly detailed. Once again, you are good at article writing and I will be coming back to view more article updates on your site.

    ReplyDelete